Andamo - Mohammed Khelef Ghassani - 書籍 - Dl2a Buluu Publishing - 9791092789256 - 2016年5月24日
カバー画像とタイトルが一致しない場合、正しいのはタイトルです

Andamo

価格
¥ 2.517
税抜

遠隔倉庫からの取り寄せ

発送予定日 年9月1日 - 年9月17日
Mohammed Khelef Ghassani の新しいリリースのお知らせを受け取る
iMusicのウィッシュリストに追加

まだ評価がありません

MUHTASARI WA KITABU: Andamo ni diwani ya tungo za ushairi zilizoandikwa na Mohammed Ghassani kwa muongo mmoja kuanzia miaka ya mwanzoni ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000. Ni tungo zinazoogelea pamoja naye kwenye bahari ya uzoefu wa mwanzo wa ujana kuelezea hadithi yake ya maisha, mtazamo wake juu ya yale yaliyokuwa yakitokea mbele ya macho yake na ufahamu wake kwa ulimwengu. Aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Fasihi na Utamaduni ya Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA), Bwana Abbas Mdungi, wakati akikabidhi ripoti ya mswaada wa diwani hii mwezi Oktoba 2003, aliandika hivi: ..".. Mshairi ameibuni kazi yake kwa ustadi mkubwa kama kwamba ni mweledi katika utunzi ilhali hii ndiyo kazi yake ya kwanza kabisa. Mitindo aliyotumia ni mingi na mizuri ambayo inatafautiana na wakati wengine kushabihiana.... Kwenye lugha, ametumia lugha ya ushairi - nyoofu, nzuri na telezi... Maudhui, bila shaka, ameyatumia vizuri kuweza kuelimisha jamii akijikita kwenye masuala ya utamaduni, siasa na uchumi, ingawa utamaduni umekuwa sura kubwa zaidi..... Kwa kawaida, washairi wa Afrika huzikita dhamira zao katika migogoro ya kimapenzi, kindoa, kidini, kikazi, kinyonyaji, kidemokrasia, uongozi mbaya, umangimeza, njaa, umasikini na maradhi, naye kwa ujumla amefanikiwa sana katika hilo...." Kwa hivyo, ndani ya Andamo, sio tu muna mwangwi wa sauti ya kijana anayejaribu kuiwasilisha hadithi yake kwa hadhira kwa njia ya kishairi, lakini pia ishara ya kuibuka kwa kipaji cha aina yake kwenye uwanja wa fasihi ya Kiswahili.

メディア 書籍     Paperback Book   (ソフトカバーで背表紙を接着した本)
リリース済み 2016年5月24日
ISBN13 9791092789256
出版社 Dl2a Buluu Publishing
ページ数 98
寸法 152 × 229 × 5 mm   ·   140 g
言語 Swahili  

同じ出版社からのその他の記事